Mzee wa miaka 84 ajinunulia jeneza kama sehemu ya maandalizi ya mazishi yake

Wakaazi katika kijiji cha Obekai Teso kusini kaunti ya Busia wamebaki vinywa wazi baada ya mzee Aloise Otieng mwenye umri wa miaka 84 kujinunulia jeneza kwa gharama ya shilingi elfu 58 kama sehemu ya mandalizi ya mazishi yake. Kulingana na mzee huyo uamuzi wa kulinunua jeneza hilo ni kuwahamasisha vijana  kuchukua jukumu la kuwalinda wazazi kama wangali hai. Hatua hiyo imekashifiwa na baadhi ya wakaazi eneo hilo huku wakisema haiendani na mila  na desturi za jamii ya Wateso.

|
News Features