Mzozo wa ardhi wazidi eneo la ziwa Naivashaadfhsdfhsfg

Mzozo unaendelea baina ya mwekezaji wa kibinafsi na baadhi ya wavuvi wa pwani ya Kamere katika ziwa Naivasha, kutokana na kile wavuvi hawa wanasema ni unyakuaji wa sehemu ya ardhi katika ziwa hilo na mwekezaji huyu.
Mzozo huu unajiri muda mchache baada ya mwekezaji huyu wa kibinafsi kuanza kuezeka ua la nyaya katika kipande hicho cha ardhi, ambalo wavuvi hawa wanasema ni mali ya umma na hakifai kumililiwa na mtu binafsi kwani sehemu hiyo inafaa kuinufaisha umma.
Wavuvi hawa wanainyoshea kidole cha lawama idara ya usalama eneo la Naivasha, wakidai maafisa wa polisi wamekuwa wakiegemea upande wa mwekezaji huyu hivyo kuwahangaisha katika jitihada za kulinda kupande hicho kisinyakuliwe.
Wanasema wamekuwa wakikamatwa na maafisa wa polisi kila mara wanapojitokeza kupinga hatua ya unyakuzi wa ardhi kwenye ziwa hilo.
 Mwa upande wake mwenyekiti wa pwani ya Kamere Wesley Kimutai amepuzilia mbali madai ya kuuzwa kwa kipande hicho cha ardhi kwa mwekezaji wa kibinafsi, akisema mwekezaji huyu ni mmoja wa wavuvi katika eneo hilo na anapania kutumia kipande hicho cha ardhi kuandaa biashara ya kuwavutia watalii.
Wazungumzaji;
 
1. Daniel Onyango, mvuvi, Kamere
2. Isaac Kigenye, mvuvi Kamere.
3. Dennis Mutheu,mvuvi Kamere.
4. Stephen Ouma, mvuvi Kamere.
5. Wesley Kimutai, mvuvi Kamere.
|
News Features